• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Taxify yabadili jina kuwa Bolt

    (GMT+08:00) 2019-03-08 19:20:00

    Kampuni inayotoa huduma za usafirishaji barani Afrika na Ulaya ya Taxify imebadilisha nembo na jina lake na kuanza kuitwa Bolt.

    Mabadiliko hayo ya alama ya utambulisho wa kampuni yamelenga kwenda sambamba na malengo ya kampuni katika huduma zake za usafiri.

    Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi mwenza wa Bolt, Markus Villig amesema jina hilo la Bolt litaanza kufahamika hatua kwa hatua katika masoko ya kimataifa katika wiki zijazo.

    Alisema Taxify ilizinduliwa miaka mitano iliyopita kwa malengo ya kutoa huduma za usafiri mijini kwa njia rahisi na bei nafuu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako