• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wakaazi zazimba walalamika uhaba wa petroli

    (GMT+08:00) 2019-03-08 19:20:39
    Wananchi visiwani hapa wamelalamikia upatikanaji usioridhisha wa mafuta aina ya petroli kwa zaidi ya siku tatu sasa.

    Baadhi ya wananchi walisema hali hiyo imesababisha usumbufu mkubwa, hasa kwa wanaotumia vyombo vya moto na abiria.

    Baadhi ya wauzaji katkavituo vya mafuta walisema hawaridhishwi na hali hiyo, lakini hawana cha kufaya hivyo wanasubiri shehena ya mafuta kutoka nje iingie.

    Hata hivyo, walilisema hali imeanza kurudi kuwa ya kawaida kwa baadhi ya vituo na wana amini mpaka kesho huenda kila kitu kikawa sawa.

    Akizungumzia hali hiyo, mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Mafuta Zanzibar (Zura), Haji Kali Haji alisema hali hiyo inatokana na kuchelewa kuingia mafuta kutoka nje kinyume cha makubaliano yao na kampuni inayohusika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako