• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vijiji vya kisasa vya China vina mustakabali mzuri

    (GMT+08:00) 2019-03-08 21:22:14

    Rais Xi Jinping wa China leo amesema, kilimo cha kisasa cha China kina fursa nyingi za kuendelezwa, na vijiji vya kisasa vina mustakabali mzuri.

    Alipozungumza na wajumbe kutoka mkoa wa Henan wanaohudhuria mkutano wa bunge la umma la China, rais Xi amesema, wahitimu wa vyuo vikuu kutoka vijijini wengi wamerudi kwenye maskani yao, vilevile watu wanaosoma nchi za nje pia wanakwenda vijijini kutafuta fursa ya kuendesha shughuli zao. Mwaka jana, China ilitoa mpango wa kwanza wa miaka mitato ya mkakati wa ustawi wa vijijini, ambao unalenga kuharakisha maendeleo ya kilimo cha China. Mpango huo unasema, inapaswa kujenga upya uhusiano kati ya miji na vijiji, haswa kuhimiza maingiliano ya watu, ardhi na mitaji kati ya miji na vijiji, ili kutia nguvu mpya katika ustawi ya vijijini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako