• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuchukua hatua mbalimbali kudumisha ukuaji wa biashara

    (GMT+08:00) 2019-03-09 13:58:04

    Waziri wa biashara wa China Bw. Zhong Shan, amesema China itachukua hatua mbalimbali za kudumisha ukuaji imara wa biashara kwa mwaka huu.

    Bw. Zhong Shan amewaambia waandishi wa habari pembezoni mwa mkutano wa bunge la umma la China, kuwa wizara ya biashara itatekeleza sera kadhaa za kuwezesha biashara na hatua za bima ya mikopo ya kusafirisha nje bidhaa, ufadhili na nyinginezo, ili kupunguza mzigo na kuboresha ufanisi kwa makampuni ya biashara ya nje.

    Amesema juhudi zitaimarishwa katika kuboresha mazingira ya biashara ili kusaidia biashara, na China itasaidia ushirikiano wa kimataifa kupitia miradi ya "Ukanda mmoja, Njia moja" na kutafuta masoko yanayoibuka, huku ikipanua masoko ya jadi. Amesema kwa jumla, China ni nchi kubwa kibiashara lakini haina ushindani wa kutosha, kwa hiyo wizara itahamasisha uuzaji nje wa bidhaa za teknolojia na ubora wa juu.

    Bw, Zhong ameongeza kuwa, kiwango cha uagizaji kitapanuliwa, na muundo wake utaboreshwa ili kukidhi mahitaji ya ndani. Wizara hiyo pia itasaidia uvumbuzi wa makampuni katika teknolojia, mifumo na usimamizi kuongeza ushindani wa soko na kuhimiza maendeleo ya biashara mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako