• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afisa wa Bunge la China asema Sheria ya Uwekezaji kutoka Nje itaongeza kiwango cha kufungua mlango

    (GMT+08:00) 2019-03-09 13:58:39

    Wakati Bunge la Umma la China linapojadili mswada wa Sheria ya Uwekezaji kutoka Nje, naibu mkurugenzi wa Kamati ya mambo ya sheria ya Halmashauri ya kudumu ya Bunge la Umma la China Bw. Liu Junchen, amesema hatua hiyo inaonesha nia na dhamira ya China kuendelea na mageuzi na kufungua mlango, na sheria hiyo itainua kiwango cha China kufungua mlango wake.

    Amefafanua kuwa, kwa mujibu wa mswada wa sheria hiyo, utawekwa aina mpya ya utaratibu wa usimamizi, kwamba wawekezaji wa nje watapata huduma sawa na kampuni za China kabla uwekezaji kuruhusiwa kuingia, na pia kutakuwa na orodha hasi.

    Afisa huyo ameongeza kuwa, sheria hiyo pia ina malengo ya kuhimiza na kulinda uwekezaji kutoka nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako