• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Israel yashambulia maeneo ya Hamas kwenye Ukanda wa Gaza

    (GMT+08:00) 2019-03-09 18:40:50
    Jeshi la Ulinzi la Israeli limetoa taarifa kuwa ndege zake zilishambulia maeneo kadhaa ya kijeshi ya kundi la Hamas kwenye Ukanda wa Gaza usiku wa Ijumaa, baada ya roketi kushambulia Israel kutoka Ukanda wa Gaza.

    Vyombo vya habari vya Israel vimesema hakuna majeruhi walioripotiwa kufuatia shambulizi hilo la roketi, baada ya kilichorushwa kuangukia kwenye eneo la wazi. Jeshi la Israeli limesema linachukulia jaribio lolote la kuwadhuru raia wa Israel kuwa ni kubwa, na itaendelea kwa dhamira kubwa kupambana na vitendo kama hivyo.

    Kwa mujibu wa wizara ya afya ya Palestina, mwandamanaji Mpalestina aliuawa kwa risasi na wengine zaidi ya 40 kujeruhiwa katika mapambano na askari wa Israel yaliyotokea Ijumaa mpakani mwa Gaza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako