• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China ashiriki kwenye mjadala wa wajumbe wa mkoa wa Fujian katika mkutano wa Bunge

    (GMT+08:00) 2019-03-11 08:52:50

    Rais Xi Jinping wa China Jumapili mjini Beijing alihudhuria mjadala wa wajumbe kutoka mkoa wa Fujian kwenye mkutano wa pili wa Bunge la awamu ya 13 la umma la China.

    Rais Xi Jinping ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati kuu ya Chama cha kikomunisti cha China na mwenyekiti wa kamati kuu ya kijeshi ya Chama, amesema China inapaswa kutafuta msukumo kutokana mageuzi na ufunguaji mlango, na kuhamasisha kikamilifu uwezo wa jamii wa kufanya uvumbuzi, ubunifu na ujasiriamali, na kuendelea kuongeza ushawishi na nguvu ya nchi kwenye ushindani katika dunia ya sasa inayoshuhudia mabadiliko makubwa.

    Rais Xi amesisitiza umuhimu wa kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya maendeleo ya vijana, na mashirika madogo na yenye ukubwa wa kati, na kuanzisha utaratibu wa kuharakisha maendeleo ya kampuni za teknolojia ya hali ya juu.

    Amehimiza utekelezaji thabiti wa sera na hatua za kuhamasisha, kuelekeza na kuunga mkono maendeleo ya sekta binafsi.

    Rais Xi amesema mkoa wa Fujian unatakiwa kutumia vyema nguvu bora ya eneo maalumu la kiuchumi, eneo la kielelezo la biashara huria, eneo la jaribio na eneo kuu la Njia ya hariri ya baharini katika Karne ya 21, na kuendelea kutafuta mbinu mpya.

    Ametoa wito wa juhudi zaidi kufanywa kutafuta njia mpya za kuhimiza maendeleo ya jumla katika kando mbili za Mlango bahari wa Taiwan.

    Rais Xi amesema kando mbili za Mlango bahari wa Taiwan zinapaswa kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara, muunganiko wa miundombinu, mabadilishano ya nishati na raslimali na kutumia vigezo vya pamoja vya viwanda.

    Rais Xi amesisitiza umuhimu wa kutekeleza dhana ya maendeleo yanayozingatia maslahi ya watu kwenye kazi kuhusu kisiwa cha Taiwan, akihimiza juhudi zifanywe ili kuwanufaisha ndugu wa Taiwan kama wanavyonufaika watu wa China bara.

    Amesema huu ni mwaka wa maadhimisho ya miaka 70 tangu China mpya ianzishwe, na ni lazima kuhakikisha hakuna mtu yeyote kwenye maeneo ya vituo vya zamani vya mapinduzi aliyeachwa nyuma kwenye mchakato wa kujenga jamii yenye maisha bora.

    Rais Xi ametoa mwito wa kuendeleza juhudi thabiti katika kupunguza umaskini na kutambua vyanzo vya umaskini, ili kuimarisha ufanisi wa hatua za kupambana na umaskini. Pia ametaka juhudi zaidi zifanywe kuratibu maendeleo ya kiuchumi na uhifadhi wa mazingira ya asili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako