• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani iko tayari kwa mkutano wa tatu na Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2019-03-11 19:10:26

    Mshauri wa masuala ya usalama wa taifa nchini Marekani Bw. John Bolton amesema, rais Donald Trump wa nchi hiyo yuko tayari kwa duru ya tatu ya mazungumzo na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un.

    Akizungumza katika mahojiano na kituo cha habari cha ABC hapo jana, Bw. Bolton amesema rais Trump yuko tayari kwa mkutano wa tatu, ingawa bado haujapangwa. Kuhusu ripoti za Korwa Kaskazini kujenga tena kituo cha majaribio ya makombora, Bw. Bolton amesema hatakisia kuhusu nini hasa picha za satelaiti zinaonyesha. Amesema Marekani haijaiuliza Korea Kaskazini kuhusu picha hizo, huku akiweka wazi kuwa ataongea na mwezake wa Korea Kaskazini kuhusu suala hilo hii leo.

    Rais Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un walifanya mkutano wao wa pili mwishoni mwa mwezi uliopita mjini Hanoi, Vietnam, lakini hawakufikia makubaliano yoyote katika mkutano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako