• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gharama ya maisha yashuka nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2019-03-11 20:56:51

    Gharama ya maisha nchini Kenya inatarajiwa kushuka ndani ya kipindi cha miezi chache ijayo kufuatia kuteremka kwa bei ya vyakula.

    Katika mwezi wa Februari mfumuko wa bei ulishuka ndani ya kipindi cha miezi sita hadi kufikia asilimia 4.1, hii ikiwa ni kutokana na kushuka kwa bei ya vyakula kama vile mahindi, mboga na sukari. Ijapokuwa bei ya mafuta inadaiwa kuteremka baada ya bei ya mafuta ghafi kuteremka katika robo ya mwaka jana, sasa huenda bei hiyo ikaanza kupanda tena kuanzia mwezi ujao.

    Wachambuzi wa biashara wanasema kuteremka kwa bei ya vyakula na mahitaji ya vyakula hivyo ni sababu tosha kwa kuzuia kupanda kwa gharama ya mafuta na kufanya mfumuko wa bei kuteremka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako