• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kamati ya Katiba na sheria ya Bunge la umma la China yapitia mswada wa Sheria ya uwekezaji wa kigeni

    (GMT+08:00) 2019-03-12 09:31:12

    Kamati ya Katiba na sheria ya Bunge la umma la China jana asubuhi ilifanya mkutano, ambapo imepitia na kujadili mswada wa Sheria ya uwekezaji wa kigeni, kutokana na maoni yaliyotolewa na wajumbe wa bunge hilo.

    Wajumbe wengi wa bunge la umma la China wameunga mkono kutunga Sheria ya uwekezaji wa kigeni. Wanaona kutunga sheria hiyo ni hatua muhimu ya kufungua zaidi mlango, kuhimiza uwekezaji wa kigeni, kukamilisha hali mpya ya ufunguaji mlango wa pande zote, na kujenga mfumo mpya wa uchumi ulio wazi.

    Vilevile wajumbe wanaona mswada huo utatoa uhakikisho wa kisheria kwa kulinda haki na maslahi halali ya wafanyabiashara wa kigeni na kuweka mazingira mazuri ya kibiashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako