• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ripoti za kazi za Mahakama Kuu na Idara Kuu ya Uendeshaji Mashtaka zinafuatilia kulinda usalama wa siasa

    (GMT+08:00) 2019-03-12 10:08:10

    Mkutano wa pili wa Bunge la 13 la Umma la China leo umeanza kujadili ripoti za kazi za Mahakama Kuu na Idara Kuu ya Uendeshaji Mashataka ambazo zote zinafuatilia kulinda usalama wa siasa wa taifa.

    Ripoti ya kazi ya Mahakama Kuu ya Umma ya China imesema mwaka jana, mahakama za ngazi mbalimbali nchini China zilitoa adhabu kali dhidi ya watu waliofanya uhalifu wa kuchochea kupindua utawala wa taifa, kuchochea kutenganisha taifa na kufanya ujasusi, na zilishirikiana na idara husika kutoa maoni ya kupambana na shughuli za kigaidi na uhalifu wa itikadi kali, kuwachukulia hatua za kisheria watu waliotetea ugaidi, kuharibu utekelezaji wa sheria kwa kutumia itikadi kali, na kulinda usalama wa siasa wa taifa haswa usalama wa utawala na usalama wa mfumo. Ripoti hiyo pia imesema mwaka huu mahakama zitatoa adhabu kali dhidi ya watu wanaoharibu usalama wa taifa, kulinda usalama wa utawala na mfumo.

    Ripoti ya kazi ya Idara Kuu ya Uendeshaji Mashtaka imesema idara za uendeshaji mashtaka za ngazi mbalimbali nchini China siku zote zinaweka kipaumbele kazi za kulinda usalama wa siasa, kupambana vikali na shughuli za kupenyaza, kupindua na kuharibu, shughuli za mabavu na ugaidi, shughuli za kutenganisha taifa na shughuli za itikadi kali za kidini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako