• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Korea Kusini yataka kufanya mazungumzo na Korea Kaskazini kuwezesha majadiliano kati ya nchi hiyo na Marekani

    (GMT+08:00) 2019-03-12 19:12:40

    Wizara ya Muungano ya Korea Kusini inayohusika na uhusiano kati ya nchi hiyo na Korea Kaskazini imesema, itafanya mazungumzo na Korea Kaskazini ili kuwezesha majadiliano kati ya Marekani na Korea Kaskazini.

    Wizara hiyo imesema, katika mpango kazi wake wa mwaka huu, uliowasilishwa ikulu ya Korea Kusini, itasukuma mbele mazungumzo kati ya nchi hiyo na Korea Kaskazini, na kupitia hayo nchi hiyo itawezesha majadiliano kati ya Marekani na Korea Kaskazini.

    Mpango kazi huo umetolewa wakati mazungumzo kati ya viongozi wa Marekani na Korea Kaskazini yaliyofanyika Hanoi, Vietnam, kumalizika bila kufikia makubaliano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako