• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Zanzibar: Benki ya PBZ yakaribisha mfumo wa kubadilisha fedha

  (GMT+08:00) 2019-03-12 19:18:16

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Ali amesema kuanzishwa kwa mfumo mpya wa ubadilishaji wa fedha za kigeni ni fursa mpya ya biashara kwa benki hiyo.

  Amesema benki hiyo imejipanga vyema na kwamba itafanya kazi hiyo ya ubadilishaji wa fedha kwa kiwango cha kisasa zaidi ili kuepusha changamoto za hapa na pale.

  Mkurugenzi huyo amesema kwa vile utaratibu wa utoaji wa huduma hiyo kwao ni mpya lakini tayari wamewaandaa wafanyakazi wao watakaohusika na huduma hiyo.

  Pamoja na hayo amesema hatua ya awali wataanza na maduka mawili ambayo yatakua eneo la Darajani Unguja na Bustani ya Forodhani huku wiki moja baadaye watasambaza maduka mengine kwenye maeneo tofauti.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako