• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito kutimiza usawa wa kijinsia

    (GMT+08:00) 2019-03-12 21:10:34

    Mkutano wa 63 wa Kamati ya Hadhi ya Wanawake ya Umoja wa Mataifa umefunguliwa katika Makao makuu ya Umoja humo mjini New York, na kuhudhuriwa na watu karibu elfu 10.

    Akizungumza katika hotuba yake ya ufunguzi, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesisitiza kuwa kufikia usawa wa kijinsia kuna manufaa kwa dunia yote.

    Mwenyekiti wa mkutano wa 73 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Bi. Maria Fernanda Espinosa amesema, bado hatua za kutosha hazijachukuliwa kuhakikisha wanawake wanashiriki kikamilifu katika masuala ya umma na kuheshimiwa kutokana na michango yao. Ameonya kwamba, kutokana na mwelekeo wa sasa, huenda malengo ya Agenda ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030 katika kufikia usawa wa kijinsia na kuongeza haki wanawake na wasichana wanazostahili hayatatimizwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako