• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Boeing yakabiliwa na hasasa kubwa baada ya mashirika ya ndege kusitisha matumizi ya ndege zake

    (GMT+08:00) 2019-03-13 08:49:21

    Thamani ya hisa ya Kampuni ya Boeing ya Marekani imeporomoka kwa zaidi ya asilimia 11 wiki hii, baada ya mamlaka za usafiri wa anga na mashirika mengi ya ndege duniani kusitisha matumizi ya ndege zake aina ya 737 Max, kufuatia ajali ya kuanguka kwa ndege ya aina hiyo nchini Ethiopia.

    Ndege aina ya Boeing 737 Max 8 ya Shirika la ndege la Ethiopia iliyokuwa ikielekea Nairobi, Kenya ilianguka Jumapili dakika chache baada ya kuruka kutoka Addis Ababa, na kusababisha vifo vya watu wote 157 waliokuwa kwenye ndege hiyo. Hiyo ni ajali ya pili ndani ya nusu mwaka baada ya ndege ya aina hiyo hiyo ya Indonesia kuanguka mwaka jana na kusababisha vifo vya watu 189.

    Mamlaka ya usafiri wa anga ya Ulaya Jumanne imetangaza kupiga marufuku matumzi ya ndege ya aina hiyo kote barani Ulaya, baada ya hatua kama hiyo kuchukuliwa na Australia, Singapore, Malaysia na China iliyokuwa nchi ya kwanza kusitisha matumizi ya ndege aina hiyo kuanzia Jumatatu.

    Hata hivyo, kampuni ya Boeing imetangaza kuwa "ina imani kamili na usalama wa ndege zake aina ya 737 Max."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako