• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa wa Umoja wa Ulaya atetea mpango wa nyuklia wa Iran kwenye baraza la usalama

    (GMT+08:00) 2019-03-13 09:37:41

    Ofisa wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia sera za kidiplomasia na usalama Bibi Federica Mogherini, jana alitetea makubaliano ya nyuklia ya Iran, akieleza mahitaji ya kuwepo kwa utaratibu thabiti wa nchi mbalimbali kutoeneza silaha za nyuklia na kuacha silaha.

    Bibi Mogherini alisema kwenye majadiliano kuhusu ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya, kuwa usalama wa pamoja unahitaji utaratibu thabiti wa nchi mbalimbali ili kutoeneza silaha za nyuklia na kuacha silaha.

    Pia amesema makubaliano ya nyuklia ya Iran yaliyofikiwa mwezi Julai mwaka 2015 kati ya Iran na Uingereza, China, Ufaransa, Ujerumani, Russia na Umoja wa Mataifa, ni mchango mkubwa kwa usalama wa pamoja na pia ni njia ya kuzuia kuenea kwa silaha za nyuklia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako