• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Suala la Brexit huenda litatatuliwa kwa haraka

    (GMT+08:00) 2019-03-13 20:08:01

    Bunge la Uingereza jana lilikata kwa mara nyingine makubaliano ya Brexit yaliyorekebishwa na serikali inayoongozwa na waziri mkuu wan chi hiyo Bi. Theresa May, ikiwa ni mara ya pili kwa bunge hilo kufanya hivyo tangu mwezi Januari mwaka huu.

    Kwa mujibu wa mpango uliopitishwa na bunge hilo mwezi Februari, kura ya moani itapigwa tena leo ili kuamua kama Uingereza itachukua hatua ya kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya bila ya makubaliano au la. Kama hatua hiyo ikikanushwa, bunge hilo litapiga kura ya maoni kuhusu ombi la kuahirisha mchakato wa Brexit kwa Umoja wa Ulaya.

    Bi. Theresa May alifanya juhudi kubwa kuhimiza bunge la nchi hiyo kupitisha makubaliano yaliyorekebishwa. Kabla ya upigaji wa kura ya maoni, alikwenda Strasbourg tena kukutana na mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Ulaya Bw. Jean-Claude Juncker, na kuomba kusahihisha kifungu cha suala la mpaka wa Ireland kwenye makubaliano hayo, ili kuondoa wasiwasi wa wabunge wanaotetea Brexit. Pande hizo mbili ziliafikiana kusaini makubaliano kuhusu uhusiano wa kibiashara kabla ya mwishoni mwa mwaka 2020, ili kuepuka "Mpango wa Uhakikisho".

    "Mpango wa Uhakikisho" unahusiana na suala la mpaka kati ya Ireland na Ireland ya Kaskazini. Kama Uingereza na Umoja wa Ulaya zikishindwa kufikia makubaliano mapya kuhusu uhusiano wa kibishara, mpaka wa Ireland na Ireland ya Kaskazini utadumisha hali ilivyo sasa. Wabunge wa Uingereza wanaotetea Brexit wana wasiwasi kuwa, hali hii italazimisha Ireland ya Kaskazini ibaki kwenye Umoja wa Ulaya, na Uingereza haitaweza kujitoa kutoka Umoja huo kihalisi.

    Baada ya bunge la Uingereza kukanusha tena makubaliano ya Brexit, Bi. May alieleza masikitiko yake, na kusema bunge hilo linapaswa kuwajibika na hatari ya kushindwa kwa Brexit. Wakati huohuo, Bw. Juncker amesema Umoja wa Ulaya hautalegeza msimamo wake mara ya tatu.

    Wachambuzi wanaona kuwa, wabunge wanaotetea au kupinga Brexit na Umoja wa Ulaya zinashikilia msimamo wao wa mwisho, na kutaka kushinikiza pande nyingine kurudi nyuma, lakini kila upande una wasiwasi mkubwa, na kutumai kufikia makubaliano mapema.

    Soko la mitaji limetambua hali hii, baada ya makubaliano ya Brexit kupingwa tena na bunge la Uingereza, kiwango cha ubadilishaji wa pound ya Kiingereza kwa dola za Kimarekani kimedumisha kuwa 1.3. Utulivu wa pound ya Kiingereza unathibitisha kuwa, watu wanaamini Uingereza itashinda kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya kwa makubaliano, ambayo huenda yatapatikana kwa haraka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako