• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Waliodanganya umri watemwa

    (GMT+08:00) 2019-03-14 07:44:06
    Chama cha Riadha cha Kenya (AK) kimewatimua kikosini wanariadha wawili chipukizi waliokuwa wakijiandaa kwa mbio za dunia za nyika zitakazofanyika jijini Aarhus, Denmark Machi 30.

    Makamu wa rais wa chama hicho, Paul Mutwii amewataja wanariadha hao ni Kibet Kandie na Agnes Mwikali waliokuwa katika vikosi vya wavulana na wasichana.

    Kulingana na Mutwii, kuondolewa kwa wawili hao kulichangiwa na udanganyifu wa umri wakati wa mchujo wa kitaifa ulioandaliwa mjini Eldoret mwishoni mwa mwezi Februari.

    Nafasi zao kwa sasa zimetwaliwa na Cleophas Kandie na Mercy Cherop. Hivi karibuni kuliibuka tetesi kwamba baadhi ya wanariadha waliowahi kuwakilisha taifa katika mashindano ya awali katika vitengo vya chipukizi walijitokeza kwa mara nyingine na vyeti ghushi vya kuzaliwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako