• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Maandalizi ya AFCON 2019 yanaendelea vizuri

    (GMT+08:00) 2019-03-14 07:44:22
    Siku 100 kuelekea fainali ya kuwania ubingwa wa soka baina ya mataifa ya Afrika nchini Misri, kamati ya maandalizi imesema maandalizi yanakwenda vizuri.

    Mwenyekiti wa kamati hiyo Hany Abo Rida ameiambia tovuti ya shirikisho la soka barani Africa (cafonline.com) kuwa, michuano hiyo itasalia katika kumbukumbu ya mashabiki wengi wa soka wakati na baada ya kumalizika.

    Misri itakuwa nchi ya kwanza, kuandaa fainali hii ambayo kwa mara ya kwanza itakuwa na mataifa 24 katika michuano itakayoanza Juni 15 hadi Julai 13 mwaka huu.

    Misri itatumia viwanja nane kwa mashindano hayo vilivyopo kwenye majiji matano tofauti: Alexandria, Ismailia, Port Said, Suez na mji mkuu wa Cairo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako