• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Ligi ya mabingwa Ulaya- Liverpool yatinga robo fainali, Barca yapiga mtu kwao

    (GMT+08:00) 2019-03-14 07:44:44
    Liverpool jana iliwafuata mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich kwa lengo moja tu kuhakikisha wanashinda na kusonga mbele hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa Ulaya.

    Kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa wiki tatu zilizopita timu hizo zilitoka suluhu uwanja wa Anfield. Katika mchezo wa jana, Liverpool imetinga robo fainali kwa kuicharaza Bayern Munich jumla ya mabao 3-1.

    Mabao ya Liverpool yamewekwa kimiani na Sadio Mane goli mbili na beki Virgil VAN Dijk aliyefunga goli moja huku Bayern wakipata bao la kufutia machozi baada ya Joel Matip wa Liverpool kujifunga.

    Mechi nyingine ilikuwa kwenye dimba laCamp Nou baina ya Barcelona wakiikaribisha Lyon ya Ufaransa, Barca wameichapa Lyon mabao 5-1. Mabao mawili yakifungwa na Lionel Messi na Phillipe Coutinho akifunga moja, huku Ousmane Dembele na Gerrald Pique wakitupia moja kila mmoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako