• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hisa za Kampuni ya Boeing matatani baada ya Marekani na Canada kusimamisha matumizi ya ndege

    (GMT+08:00) 2019-03-14 08:57:34

    Hisa za kampuni ya ndege ya Boeing ya Marekani zilishuka jana baada ya Marekani na Canada kuamua kwa pamoja kuzuia ndege zake aina ya Boeing 737 Max kuruka.

    Jumatano baada ya masoko ya hisa kufunguliwa hisa za kampuni hiyo zilikuwa na mwelekeo mzuri, na kupanda kwa asilimia 1.6, lakini thamani yake ilianza kupungua baada ya Marekani na Canada kutangaza uamuzi wao.

    Marekani imefikia uamuzi huo baada ya Rais Donald Trump kuamuru hivyo, uamuzi alioutoa baada ya Canada kufanya uamuzi kama huo. Marekani na Canada zinaungana na nchi na sehemu mbalimbali duniani ikiwemo China, Umoja wa Ulaya na Indonesia, ambazo pia zimefanya uamuzi kama huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako