• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wajumbe wanaoshiriki kwenye Mikutano Miwili ya China wakaribisha hotuba aliyoitoa rais Xi Jinping wa China

    (GMT+08:00) 2019-03-14 17:09:00

    Katika Mikutano Miwili inayoendelea nchini China, rais Xi Jinping wa China, pamoja na wajumbe wa bunge la umma la China na Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China, wamefanya mijadala mingi kuhusu masuala yanayofuatiliwa zaidi na watu ukiwemo ujenzi wa ustaarabu wa ikolojia, uondoaji wa umaskini, ustawishaji wa vijiji na uboreshaji wa mazingira ya biashara. Hivi sasa China inahimiza kwa nguvu zote ujenzi wa ustaarabu wa ikolojia. Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani ni eneo muhimu lililoko kaskazini mwa China katika kulinda usalama wa ikolojia. Rais Xi aliposhiriki kwenye mjadala na wajumbe kutoka Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani amesema, inapaswa kuongeza nguvu katika kulinda utaratibu wa ikolojia, na kushughulikia vizuri kazi ya kuzuia uchafuzi wa mazingira. Rais Xi anasema:

    "Haipaswi kuharibu mazingira ya ikolojia kutokana na kukabiliwa na matatizo fulani ya kiuchumi. Wakati uchumi wa nchi yetu unapobadilika kutoka kipindi cha kupata ongezeko la kasi hadi kupata maendeleo yenye ubora mzuri, kukinga na kushughulikia uchafuzi wa mazingira ni kazi muhimu. Tunapaswa kushinda tatizo hilo, na kuimarisha nguvu katika kulinda mazingira ya ikolojia kwa nia thabiti."

    Kuwasaidia watu maskini na kustawisha vijiji vilevile ni jambo linalofuatiliwa na rais Xi. Aliposhiriki katika mjadala na wajumbe wa Mkoa wa Henan, rais Xi amesisitiza kipaumbele katika kutekeleza mikakati ya kustawisha vijiji ni kuhakikisha mazao ya kilimo haswa utoaji wa chakula. Mjumbe wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China ambaye pia ni naibu mkuu wa Chuo cha Sheria kwenye Chuo Kikuu cha Fedha cha Guangdong Bw. Lu Xiaoming anaona kuwa, maneno hayo ya rais Xi yameonesha mwelekeo wa ustawishaji wa vijiji. Anasema:

    "Matatizo yanayoukumba ustawishaji wa mambo ya vijijini na upande wa maendeleo yote yamehusishwa kwenye maagizo aliyoyatoa rais Xi. Naamini kuwa maelekezo hayo ya rais Xi yatahimiza ustawishaji wa mambo ya vijijini. "

    Namna ya kuhimiza kampuni za watu binafsi kupata maendeleo yenye ubora mzuri vilevile ni suala linalofuatiliwa wakati wa Mikutano Miwili. Rais Xi amesisitiza kwenye mjadala kati yake na wajumbe wa mkoa wa Fujian, kuwa inapaswa kutekeleza sera na hatua mbalimbali za kuelekeza kampuni za watu binafsi kupata maendeleo ya kiuchumi, na kuweka mazingira yaliyo na usawa, uwazi na kufuata utaratibu wa sheria kwa kampuni hizo. Mjumbe wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China Bw. Wei Mingde anasema:

    "Nimetiwa moyo kutokana na maagizo aliyoyatoa rais Xi kuhusu kujenga mazingira mazuri ya kibiashara. La muhimu zaidi ni kuhakikisha mazingira ya ushindani yenye usawa na uwazi, kwa mfano watu wanaweza kuona hatua zote za kukaguliwa kupitia mtandao wa Internet."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako