• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la chini la bunge la Uingereza lapiga kura kupinga kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya bila ya makubaliano

    (GMT+08:00) 2019-03-14 17:21:28

    Baraza la chini la bunge la Uingereza jana limepiga kura na kupinga nchi hiyo kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya bila ya makubaliano katika wakati wowote.

    Baraza hilo pia limepitisha marekebisho yasiyo ya kisheria kuhusu kupinga kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya bila ya makubaliano katika wakati wowote kwa kura 312 za ndiyo dhidi ya kura 308 za hapana.

    Aidha, baraza hilo lilipiga kura tena na kupitisha pendekezo la serikali la kisheria kwa kura 321 za ndiyo dhidi ya kura 278 za hapana, ambalo limeweka bayana kupinga kujitoa Umoja wa Ulaya bila ya makubaliano. Wakati huo huo, baraza hilo limepiga kura na kukataza marekebisho kuhusu kuahirisha Brexit hadi tarehe 22 mwezi Mei.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako