• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uingereza yakataa kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya bila ya makubaliano

    (GMT+08:00) 2019-03-14 19:46:19

    Bunge la Uingereza juzi lilipiga kura kukataa marekabisho ya makubaliano ya Brexit yaliyotolewa na serikali ya Theresa May, na jana, bunge hilo limekanusha tena pendekezo la kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya bila ya makubaliano.

    Maana ya Kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya bila ya makubaliano ni kwamba, kama Uingereza ikishindwa kusaini makubaliano ya Brexit na Umoja wa Ulaya kabla ya Machi 29, makubaliano yote yaliyofikiwa na pande hizo mbili yatafutwa. Baada ya kujitoa kutoka Umoja huo, Uingereza haitakuwa na kipindi cha mpito, na sheria za Umoja wa Ulaya hazitatumika tena Uingereza. Uhusiano kati ya Uingereza na Ulaya utarudi katika utaratibu wa Shirika la Biashara Duniani (WTO), na pande hizo mbili zitakabiliwa na suala la ongezeko la kiwango cha ushuru na vikwazo vya kibiashara.

    Ni dhahiri kwamba kwa kulinganishwa na mipango miwili ya makubaliano ya Brexit na kuahirisha kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya, kujitoa kutoka Umoja huo bila ya makubaliano ni chaguo baya zaidi kwa pande hizo mbili. Hivyo, mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Ulaya Bw. Jean Claude Juncker amesema, kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya bila ya makubaliano ni maafa makubwa ambayo kamati hiyo imejaribu kuzuia. Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Bw. Jeremy Hunt pia amesisitiza kuwa kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya bila ya makubaliano kutaleta athari kubwa kwa uhusiano kati ya Uingereza na nchi za Umoja wa Ulaya, ambayo pia ni kosa kubwa la kimkakati la kijiografia.

    Bw. Hunt aliwahi kusema, baadhi ya watu wa Umoja wa Ulaya wanaona kuwa kama wakisubiri kwa muda wa kutosha, Uingereza itarudi nyuma. Lakini Umoja wa Ulaya, kundi linalotaka Uingereza ijitoe kwenye Umoja huo, na kundi linalotaka ibaki kwenye Umoja huo nchini Uingereza zote haziwezi kuzilazimisha pande nyingine kurudi nyuma na kulinda maslahi yao. Hivyo matokeo yatakuwa kwamba mapendekezo yanakataliwa, lakini pande mbalimbali haziwezi kufikia makubaliano, kwa sababu pande hizo zinajua vitu wasivyovitaka, lakini haziwezi kueleza vitu wanavyovitaka. Katika mchakato wa ushindani, jamii ya Uingereza inaendelea kutengwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako