• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Serikali yapanga kudhibiti nauli za magari ya uchukuzi wa umma

    (GMT+08:00) 2019-03-14 20:07:22

    Huenda abiria wanaotumia usafiri wa umma nchini Kenya wakapata ahueni ya nauli iwapo bunge litapitisha marekebisho ya Sheria ya Trafiki na ile ya Mamlaka ya Kitaifa ya Usalama Barabarani na serikali kuanza kukadiria na kusimamia naili zinazotozwa na magari ya uchukuzi wa umma.

    Katika taarifa iliyowasisilishwa bungeni na Waziri wa Uchukuzi James Macharia,wziri huyo alisema hatua hiyo inalenga kuwalinda wananchi dhidi ya wenye magari kuongeza nauli kiholela.

    Aidha alisema Wizara yake itawasilisha mapendekezo hayo kwa baraza la mawaziri kabla ya kuwasilishwa bungeni.

    Wizara hiyo ya uchukuzi inapendekeza kudhibiti nauli za magari ya uchukuzi wa umma kwa kuifanyia marekebisho sehemu ya 119 (1) ya Sheria ya Trafiki kwa kuanzisha ibara nyingine ambayo itamruhusu Waziri wa Uchukuzi kufanya maamuzi hayo.

    Iwapo marekebisho hayo ya sheria yatapitishwa waziri atakuwa na uwezo wa kisheria wa kubaini mfumo wa kuweka mwongozo kuhusu nauli, mbinu za kubadilisha viwango vya nauli na kuweka adhabu kwa wale ambao watakiuka mwongozo huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako