• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Mary Njoroge ateuliwa kusimamia mechi za AFCON U-17

    (GMT+08:00) 2019-03-15 07:48:35
    Mshika kibendera wa Kenya Mary Njoroge ameteuliwa katika orodha ya wasimamizi 19 watakaosimamia mechi za wachezaji wanaume kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 yatakayofanyika nchini Tanzania.

    Uamuzi wa kuanza kutumia marefa wanawake katika mashindano ya wanaume ulifikiwa baada ya kamati ya marefa ya shirikisho la soka barani Afrika (CAF) katika kikao kilichofanyika Februari 26 mwaka huu makao makuu jijini Cairo nchini Misri na kuhudhuriwa na rais wa CAF, Ahmad Ahmad.

    Marefa 15 na wasaidizi wao wa pembeni ambao ni washika vibendera 14 kutoka mataifa 25 wanachama, watafanyiwa ukaguzi wa kiafya, mazoezi ya uwanjani na pia kufanya mtihani ili kupata orodha ya mwisho ya maafisa wa kusimamia mechi wakati wa mashindano hayo yatakayoanza Aprili 14-28 mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako