• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Netanyahu aitisha majadiliano ya kijeshi baada ya shambulizi la maroketi kutoka Gaza

    (GMT+08:00) 2019-03-15 09:15:48

    Waziri mkuu wa Israel Bw. Benjanin Netanyahu jana usiku aliitisha majadiliano ya dharura ya kijeshi na makamanda wa jeshi nchini humo, baada ya shambulizi la maroketi dhidi ya Tel Aviv kutoka Gaza.

    Jeshi la Israel limesema, maroketi mawili yalirushwa kutoka Gaza. Na mtoto wenye umri wa miaka 10 na mwanaume wenye umri wa miaka zaidi ya 50 walijeruhiwa kwenye shambulizi hilo na kupata matibabu. Hakuna kundi lolote lililotangaza kuwajibika na shambulizi hilo.

    Hii ni mara ya kwanza kwa Tel Aviv kushambuliwa kwa maroketi tangu mwaka 2014, Israel ilipofanya operesheni ya kijeshi kwenye ukanda wa Gaza.

    Habari pia zinasema leo alfajiri ndege za kivita za Israel zimefanya mashambulizi kujibu mashambulizi hayo ya maroketi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako