• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wayemen wafanya mazishi kwa watu 22 waliouawa katika mashambulizi ya anga ya Saudi Arabia

    (GMT+08:00) 2019-03-15 09:50:28

    Maelfu ya Wayemen wamekusanyika katika mji mkongwe wa kihistoria wa Sanaa kwenye mazishi ya watu 22 waliouawa katika mashambulizi ya anga ya muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia. Kwa mujibu wa wakazi na hospitali, ndege za kivita zilishambulia nyumba kadhaa katika eneo lenye mgogoro la Kushar, mkoani Hajjah, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo. Mratibu wa mambo ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Lise Grande, amesema mashambulizi hayo yalisababisha vifo vya wanawake 10 na watoto 12, na kuwajeruhi watu wengine 30, wakiwemo 14 walio na umri wa chini ya miaka 18.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako