• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uongozi wa China duniani wapata uungaji mkono zaidi kuliko Marekani

    (GMT+08:00) 2019-03-15 10:22:42

    Ripoti mpya iliyotolewa na kampuni ya Gallup inaonesha kuwa, mwaka jana uongozi wa China ulipata asilimia 34 ya uungaji mkono duniani, ambao ni mkubwa zaidi kuliko Marekani, na mkubwa zaidi katika karibu miaka 10 iliyopita.

    Ripoti hiyo imetathmini maoni ya umma kuhusu uongozi wa Marekani, China, Ujerumani na Russia duniani. Uungaji mkono kwa Marekani umepungua kuwa asilimia 31, mdogo zaidi ukilinganishwa na ule wa serikali za awamu tatu zilizopita za Marekani.

    Russia ilipata asilimia 30 ya uungaji mkono, na hii ni mara ya kwanza kwa Russia kupata uungaji mkono sawa na Marekani. Uungaji mdogo wa Marekani huenda utaathiri nguvu yake laini. Hii inamanisha kuwa hali isiyokadiriwa na kutotimiza ahadi wa serikali inayoongozwa na rais Donald Trump, imesababisha mashaka kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako