• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mjadala bungeni kuhusu mayai milioni 33 kutoka Uchina

  (GMT+08:00) 2019-03-15 19:29:05
  Wizara ya Kilimo ya Kenya imesema kampuni za ujenzi za Uchina zinaingiza nchini Kenya mamilioni ya mayai. Ilibainika kuwa katika kipindi cha miaka miwili, zaidi ya mayai milioni 33 yameingizwa nchini kutoka Uchina.

  Serikali imekuwa ikiruhusu kampuni za uchina ambazo zimepewa kandarasi za kutengeneza barabara kuingiza mayai nchini.

  Kulingana na ripoti hiyo ya wizara, mnamo 2017, Kenya iliingiza mayai milioni 15 kutoka mataifa mbalimbali ya kuanguliwa vifaranga na kuliwa.

  Mayai yote ya kuliwa yalitoka Uchina, yakiingizwa na kampuni za Sinohydro Corporation Ltd, Chia Town Supermarket Ltd, Seven Days International (K) Ltd na Ling Yue International CO Ltd.

  Ripoti hiyo ilizua mjadala mkali miongoni mwa wabunge, ambao walishangaa sababu ya serikali kuruhusu mayai kuingizwa kutoka nje, wakati tayari kuna mayai ya kutosha Kenya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako