• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mpango wa serikali kupunguzia wananchi nauli

  (GMT+08:00) 2019-03-15 19:29:47

  Serikali ya Kenya itaanza kukadiria na kusimamia nauli zinazotozwa na magari ya uchukuzi wa umma kote nchini humo ikiwa bunge litalipitisha marekebisho kwa Sheria ya Trafiki na ile inayosimamia Mamlaka ya Kitaifa ya Usalama Barabarani (NTSA).

  Waziri wa Uchukuzi James Macharia aliwaambia wabunge kwamba hatua hiyo inalenga kukinga wananchi dhidi ya kupunjwa na wenye magari hayo kupitia nyongeza za nauli kiholela.

  Bw Macharia alisema kuwa wizara yake itawasilisha mapendekezo hayo kwa baraza la mawaziri kabla ya kuwasilishwa bungeni.

  Wizara hiyo ya uchukuzi inapendekeza kuifanyia marekebisho sehemu ya 119 (1) ya Sheria ya Trafiki kwa kuanzisha idara nyingine ambayo itamruhusu Waziri wa Uchukuzi kuamua namna nauli za magari ya uchukuzi yatadhibitiwa.

  Marekebisho hayo ya sheria yakipitishwa waziri atakuwa na uwezo wa kisheria wa kubaini mfumo wa kuweka mwongozo kuhusu nauli, mbuni za kubadilisha viwango vya nauli na kuweka adhabu kwa wale ambao wakakiuka mwongozo huo.

  Wizara hiyo vile vile inapania kufanyia marekebisho sehemu ya 4(2) ya Sheria ya NTSA kwa kuanzisha idara mpya itakayotoa nafasi kwa asasi hiyo kuanzisha mwongozo wa nauli ya magari ya uchukuzi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako