• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa mazingira wa UN wafungwa huku mwongozo mpya wa mustakabali endelevu ukipitishwa

    (GMT+08:00) 2019-03-16 17:08:23

    Mkutano wa nne wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA umefungwa jana huku wajumbe wakipitisha mwongozo wa kukuza hatua endelevu ambazo zitaondoa madhara duniani na kwenye rasilimali zake.

    Wajumbe kutoka zaidi ya nchi 170 wanachama wa Umoja wa Mataifa wameahidi kuunga mkono kutumia haraka na vizuri uvumbuzi na hatua zinazohitajika katika kupambana na changamoto za mazingira kama vile mabadiliko ya hali ya hewa, taka za plastiki na kupoteza makazi, na kusaidia jamii kusonga mbele na kuingia kwenye siku zisizo na uchafuzi wa mazingira na endelevu.

    Kwenye tamko lao la pamoja wajumbe hao pia wamethibitisha kuwa kutokomeza umasikini, kukuza mfumo endelevu wa matumizi na uzalishaji, kulinda na kusimamia maliasili chini ya msingi wa maendeleo ya uchumi na jamii kuwa ni malengo yatakayofikiwa, na ni mahitaji ya lazima kwa maendeleo endelevu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako