• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya watu waliouawa kwenye shambulizi la kigaidi New Zealand yaongezeka na kufikia 50

    (GMT+08:00) 2019-03-18 08:50:49

    Polisi nchini New Zealand wamesema idadi ya watu waliouawa kwenye shambulizi la kigaidi, imeongezeka na kufikia 50 baada ya mhanga mmoja zaidi kupatikana kwenye moja ya maeneo ya shambulizi.

    Wachunguzi walipata mwili huo kwenye msikiti wa Masjid Al Noor ambapo watu zaidi ya 40 waliuawa baada ya kushambuliwa Ijumaa iliyopita. Idadi ya watu waliojeruhiwa imetajwa kuwa ni 50, na 36 kati yao wanaendelea kutibiwa katika hospitali ya Christchurch.

    Waziri Mkuu wa New Zealand Bibi Jacinda Arden amesema kuwa miili ya waliouawa inarudishwa kwa familia, lakini hadi sasa ni miili michache tu ndio iliyorudishwa kwenye familia zao.

    Kufuatia tukio hilo, waziri mkuu Bibi Jacinda Arden amesema sheria za umiliki wa silaha nchini New Zealand zitabadilishwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako