• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KIKAPU: Droo ya mechi za kombe la dunia mchezo wa Kikapu yafanyika

    (GMT+08:00) 2019-03-18 09:12:49

    Matokeo ya droo ya upangaji makundi ya timu zinazoshiriki michuano ya kombe la dunia mwaka huu ya mchezo wa mpira wa kikapu imefanyika mwishoni mwa juma mjini Shenzhen.

    Droo hiyo imeongozwa na Wakongwe Wawili (Balozi wa Kombe la dunia 2019 Kobe Bryant pamoja na Rais Chama cha mchezo wa Basketball China Yao Ming)

    Katika droo hiyo wenyeji China wamepangwa kundi A pamoja na timu za Ivory Coast kutoka Afrika, Poland ya Ulaya na Venezuela ya Amerika Kusini na mechi za kundi hili zote zitafanyika mjini Beijing.

    Mashindano kombe la dunia yatafanyika Agosti 31-Septemba 15 katika miji 8 ya China.

    Pamoja na Ivory Coast Washindani wengine kutoka Afrika ni Angola, Nigeria, Senegal na Tunisia.

    Na Siku ya kwanza ya mashindano hayo Agosti 31 kutachezwa mechi 16, Ivory Coast watacheza na wenyeji China kwenye uwanja wa Cadillac Arena mjini Beijing.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako