• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Agizo la Rais Kenyatta laleta matumaini kwenye sekta ya michezo

    (GMT+08:00) 2019-03-18 09:18:29

    Agizo la rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta kuwa timu zote za kitaifa zitakazowakilisha Kenya katika mashindano ya kimataifa zifadhiliwe na serikali limeanza kutekelezwa.

    Rais wa shirikisho la soka nchini humo (FKF) Nick Mwendwa ameweka wazi kuwa serikali ya Kenya inaanza kutekeleza ahadi yake kwa kuwekeza zaidi ya shilingi milioni 240 kwenye michezo.

    Mwendwa amesema Serikali imethibitisha kuwa wiki hii itaikabidhi timu ya taifa ya mpira wa miguu (Harambee Stars) kiasi cha shilingi milioni 50 za Kenya. pesa hizo zitatumika kutekeleza shughuli za soka, ikiwa ni pamoja na kuandaa timu kwaajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2019 zinazofanyika Misri.

    Akizungumza mwishoni mwa makala ya nne ya mbio za Beyond Zero Marathon wikendi iliyopita, Rais aliwahakikishia wanamichezo kuwa serikali yake itafadhili vikosi vyote vitakavyowania mataji mbalimbali katika majukwaa ya kimataifa.

    Kenya ambayo ina pointi 7 ikiongoza Kundi F lenye timu za Ghana na Ethiopia imeshafuzu tayari hivyo itacheza mchezo wa kuamua nani awe kinara wa kundi hilo dhidi ya Ghana yenye pointi 6, Machi 23.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako