• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • LANGALANGA 2019: Mashindano yafunguliwa kwa mbio za kwanza nchini Australia

    (GMT+08:00) 2019-03-18 09:18:51

    Valterri Bottas wa timu ya Mercedes ambaye raia wa Finland amefanikiwa kushinda ubingwa wa mbio za kwanza kwa mwaka huu za magari ya mashindano ya mwendokasi zilizofanyika nchini Australia.

    Bottas aliwashinda madereva wenzake 19 baada ya kutumia saa 1 dakika 25 na sekunde 27 katika mizunguko 58 ya mbio hizo zilizofanyika mjini Melbourne.

    Nafasi ya pili kwenye mbio hizo imechukuliwa na mwingereza Lewis Hamilton ambaye ni kutoka timu ya mercedes pia. Na nafasi ya tatu imekwenda kwa mholanzi Max Verstappen wa timu ya Red Bull.

    Madereva hao sasa wanajiandaa tena kwa ajili ya mbio za pili zitakazofanyika machi 31 nchini Bahrain.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako