• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa waraka kuhusu kupambana na ugaidi na ulinzi wa haki za binadamu Xinjiang

    (GMT+08:00) 2019-03-18 10:23:08

    Ofisi ya habari ya baraza la serikali la China imetoa waraka kuhusu mapambano dhidi ya ugaidi na siasa kali, na ulinzi wa haki za binadamu mkoani Xinjiang.

    Waraka huo umesema serikali ya China imesimama kidete kupinga aina zote za ugaidi na siasa kali, na haisiti kupambana vikali kwa mujibu wa sheria, na vitendo vyote vya kuhimiza ugaidi na siasa kali, na vitendo vinavyohusu kuratibu, kupanga na kutekeleza shughuli za kigaidi, au kukiuka haki za binadamu.

    Waraka huo pia umesema Xinjiang ni sehemu isiyotengeka ya ardhi ya China, na tamaduni za kikabila za Xinjiang ni sehemu isiyotengeka ya ustaarabu wa China. Waraka huo umesema kuwa watu wa kabila la Uygur wamekuwepo kutokana na mchakato wa uhamiaji na maingiliano ya kikabila, na wao sio vizazi vya waturuki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako