• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kununua Ovacado kutoka Kenya

    (GMT+08:00) 2019-03-18 19:11:58

    Wizara ya kilimo nchini Kenya inalenga kuwasaidia wakulima wa zao la Ovacado kupata soko nchini China.Meneja wa tume ya kukagua ubora wa mimea nchini Kenya Kephis Esther Kimani amesema tayari amewaalika wataalam kutoka China kufanyia ukaguzi bidhaa hiyo wakati wa msimu wa mavuno.

    Hii ni mojawapo ya mapendekezo yaliyotolewa na China kabla ya kufungua soko la Ovacado kwa Kenya nchini China. Ukaguzi huo utakuwa ni kuangalia mchakato mzima kuanzia jinsi yanavyovunwa na upakiaji. Wataalam hao wa China watahifadhiwa kwenye mashamba ya Ovacado katika maeneo ya Kakuzi,Embu, Muranga,Uasin Gishu na Tranzoia kabla ya kupelekwa kwenye uwanja wa ndege kuangalia jinsi ukaguzi wa matunda hayo unavyofanywa. Hatua hiyo inafuatia ombi la muda mrefu la Wachina kutaka kusafirishwa kwa Ovacado nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako