• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka Marekani kusikiliza maoni halisi ya waafrika na kutoa mchango halisi kwa Afrika

    (GMT+08:00) 2019-03-18 19:11:53

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amepinga kauli iliyotolewa na msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Tibor Nagy kuhusu ushirikiano kati ya China na Afrika. Bw. Geng Shuang amesisitiza kuwa, China siku zote inafanya ushirikiano na Afrika kwa mawazo ya kidhati, na inazingatia maoni sahihi ya kunufaishana. Amewataka maofisa wa ngazi ya juu wa Marekani kusikiliza maoni halisi ya waafrika na kutoa mchango halisi kwa Afrika.

    Hivi karibuni akiwa nchini Uganda, msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Nagy alisema mafanikio ya ushirikiano kati ya China na Afrika sio makubwa kama yanavyoelezwa, na kwamba mikopo ya China imeongeza mzigo wa madeni wa Afrika.

    Bw. Geng Shuang amesema, kuna ushahidi dhahiri kuwa mafanikio ya ushirikiano kati ya China na Afrika yanawanufaisha waafrika katika sekta mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako