• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Xinjiang kusukuma mbele miradi ya kunufaisha watu katika sekta za ajira, elimu, matibabu na bima ya umma

    (GMT+08:00) 2019-03-18 19:36:19

    Ofisi ya habari ya baraza la serikali la China imetoa waraka kuhusu mapambano dhidi ya ugaidi na msimamo mkali, na ulinzi wa haki za binadamu mkoani Xinjiang.

    Waraka huo umesema, katika miaka ya hivi karibuni mkoa wa Xinjiang umetekeleza wazo la kuzingatia watu, kuhakikisha na kuboresha maisha ya watu, na kusukuma mbele kwa nguvu kubwa miradi ya kunufaisha watu katika sekta za ajira, elimu, matibabu na bima ya umma.

    Kwa mujibu wa waraka huo, Xinjiang inatekeleza mpango wa kutoa ajira kwa watu laki moja wa kusini mwa mkoa huo kati ya mwaka 2018 hadi mwaka 2020, na mpaka sasa imesaidia watu elfu 75 zenye hali mbaya ya kiuchumi kupata ajira. Mkoa huo pia umejitahidi kueneza elimu ya miaka 9 bila malipo, kutekeleza upimaji wa afya bila malipo na bima ya matibabu ya magonjwa makubwa, kuboresha mfumo wa huduma za umma, na kuinua kigezo cha kuhakikisha maisha ya watu juu ya kiwango cha msingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako