• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Data za kisanduku cheusi zaonesha "kufanana wazi" kwa ajali za ndege za Ethiopia na Indonesia

    (GMT+08:00) 2019-03-19 08:43:21

    Mamlaka ya uchunguzi wa usalama wa ndege ya Ufaransa (BEA), inayofanya uchunguzi wa chanzo cha ajali ya hivi karibuni ya ndege ya shirika la ndege la Ethiopia aina ya Boing 737 Max, imesema imegundua hali ya kufanana kwa ajali ya ndege ya Ethiopia na ile ya shirika la ndege la Lion Air la Indonesia iliyoanguka kwenye bahari Oktoba mwaka jana.

    BEA imesema wakati wa kuchambua data zilizotolewa kwenye kisanduku cheusi, wachunguzi wamegundua hali wazi ya kufanana, na data hizo zitafanyiwa uchunguzi zaidi. Ripoti ya awali kuhusu matokeo ya uchunguzi itatolewa ndani ya siku 30. Wakati wakisubiri matokeo kamili ya uchunguzi, kurugenzi ya usafiri wa ndege ya Ufaransa, pia imepiga marufuku ndege aina ya Boeing 737 Max kuruka kwenye anga ya nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako