• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kufuzu Afcon 2019: Uganda waweka kambi Misri kujiwinda na mechi ya mwisho dhidi ya Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-03-19 09:10:43

    Timu ya taifa ya Uganda imesafiri hadi nchini Misri kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya mwisho ya hatua ya makundi ya kufuzu mashindano ya Afrika AFCON itakayochezwa machi 23 mjini Dar es Salaam dhidi ya Tanzania.

    Uganda ambao hata hivyo tayari wamefuzu tayari kwa mashindano hayo yatakayofanyika mwezi juni nchini Misri, wanaongozwa na kocha Sebastien Desabre ambaye amewaita kikosini wachezaji nyota wanaocheza soka la kulipwa nje ya Uganda.

    Nako nchini Tanzania, wachezaji nyota wanaocheza nje ya nchi wameendelea kuwasili nchini humo ili kujiwinda na mechi hiyo ambayo kwao ushindi ni lazima ili waweze kufuzu.

    Kocha mkuu wa timu hiyo Emanuel Amunike ameendelea kufanya mabadiliko katika kikosi chake ili kuongeza uwezo wa ufanisi ikiwemo ya hivi karibuni kwa kumwita mlinzi wa klabu ya Simba Erasto Nyoni.

    Katika kundi lao hilo, Uganda inaongoza kwa kuwa na alama 13, ikifuatiwa na Lesotho yenye alam a 5, Tanzania ina alama 5 pia katika nafasi ya tatu na Cape Verde ikio nafasi ya 4 kwa kuwa na alama 4

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako