• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashindano ya Ethiopia: Rwanda na Eritrea washinda ubingwa wa Afrika kwa vijana.

    (GMT+08:00) 2019-03-19 09:12:32

    Mwendesha baiskeli wa Rwanda Renus Byiza Uhiriwe amefanikiwa kupeperusha vyema bendera ya taifa lake baada ya kushinda ubingwa wa mashindano ya vijana ya Afrika yiliyofanyika nchini Ethiopia.

    Uhiriwe aliwashinda baada ya kutumia saa 2 dakika 30 na sekunde 23 kwenye umbali wa kilomita 104.4 katika mzunguko wa mwisho, na kwa ushindi huo alizawadiwa medali ya dhahabu na kutangazwa kuwa ndiye bingwa wa Afrika kwa vijana.

    Mshindi wa pili katika mashindano hayo ni Yoel Asmeron wa Ertitrea na mshindi wa tatu ni Yowhanes Gebrihiwet wa kutoka Ethiopia.

    Lakini kwa upande wa wanawake Diane Ingabire wa Rwanda alishinda nafasi ya pili huku nafasi ya kwanza ikichukuliwa na Danait Tsegay wa Eritrea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako