• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kufuzu ubingwa wa Afrika: Magereza Wanawake kutoka Kenya yaendeleza ushindi wa asilimia 100

    (GMT+08:00) 2019-03-19 09:13:24

    Timu ya Magereza wanawake kutoka Kenya imefanikiwa kuifunga timu ya Nkumba University kutoka Uganda kwenye mechi ya kufuzu fainali za Afrika katika mchezo wa mpira wa wavu.

    Katika mechi hiyo iliyofanyika mjini Cairo, Magereza Kenya ushindi wa seti 3-1 na kuwafanya washikilie rekodi ya asilimia 100 katika mechi walizocheza.

    Kutokana na ushindi huo mabingwa hao wa Kenya wanahitaji kupata ushindi mmoja tu katika mechi zao mbili zilizosalia ili kufuzu kutoka kundi D, ambapo wanatarajiwa kucheza na El Shams ya Misri na GSP ya Algeria.

    Aidha katika mechi zilizopita Magereza walipata ushindi dhidi ya Asec ya Ivory Coast na RRA ya Rwanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako