• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chipukizi wawapigisha kwata mabingwa na kuchukua ubingwa.

    (GMT+08:00) 2019-03-19 09:13:43

    Mchezaji tennis wa Austria Dominic Thiem ameshinda ubingwa wa mashindano ya Indian Wells nchini Marekani kwa kumfunga bingwa wa kihistoria kwenye mchezo wa tennis Roger Federer wa Uswisi katika mchezo wa fainali uliofanyika jana.

    Thiem ambaye anashika nafasi ya saba kwa ubora, ameshinda kwa seti yenye alama 3-6 6-3 na 7-5, na kutokana na ushindi huo ubora atapanda kwa viwango vya ubora hadi kufikia nafasi ya nne.

    Kwa upande wa wanawake mchezaji ambaye ni bingwa mara tatu wa michuano mikubwa, Angelique Kerber amejikuta akifungwa katika fainali ya Indian Wells na mchezaji chipukizi Bianca Andreescu wa Romania kwa seti yenye alama 6-4 3-6 6-4.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako