• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FC Barcelona imethibitisha kuwa Luis Suarez atakuwa nje ya dimba kwa siku kadhaa

    (GMT+08:00) 2019-03-19 09:14:06

    Club ya FC Barcelona ya Hispania jana imetangaza rasmi kuwa mshambuliaji wake wa kimataifa wa Uruguay Luis Suarez watamkosa katika michezo kadhaa kufuatia majeraha aliyoyapata katika mchezo wa ligi kuu ya Hispania (La Liga) dhidi ya Real Betis.

    Barca walimtoa Suarez uwanjani dakika za mwisho wakati wa mchezo dhidi ya Real Betis uliyomalizika kwa Barcelona kupata ushindi wa magoli 4-1,huku katika mchezo huo, Luis Suarez alifunga goli lake la 18 la LaLiga.

    Kutokana na majeraha aliyoyapata, Barca wametangaza kuwa Suarez atakuwa nje ya uwanja kwa siku kati ya 10 hadi 15, pamoja na kuwa aliitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uruguay kutokana na kuumia kifundo cha mguu ameondolewa kikosini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako