• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Ulaya zafanya duru ya tisa ya mazungumzo ya ngazi ya juu ya kimkakati

    (GMT+08:00) 2019-03-19 09:33:23

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi na ofisa wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia sera za kidiplomasia na usalama Bibi Federica Mogherini, jana wameendesha kwa pamoja duru ya tisa ya mazungumzo ya ngazi ya juu ya kimkakati kati ya China na Ulaya mjini Brussels.

    Bw. Wang Yi amesema China na Ulaya ni wenzi wa kimkakati wa pande zote, kuna uwezekano mkubwa wa ushirikiano kati ya pande mbili. Amesisitiza kuwa wenzi wa ushirikiano ni kitu cha kimsingi kwa uhusiano kati ya China na Ulaya, kunufaishana ni lengo la ushirikiano kati ya pande mbili, kuheshimiana maslahi makuu ni ishara ya uaminifu kati yao. Amesema China inapenda kushirikiana na Ulaya katika kulinda na kuendeleza uhusiano kati ya pande mbili na kuwanufaisha watu wao.

    Kwa upande wa Ulaya, Bibi Mogherini amesema Ulaya inaichukulia China kuwa ni mwenzi wake muhimu wa kimkakati siku zote, na inapenda kushirikiana na China katika kuhimiza utekelezaji wa makubaliano ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako