Kamisheni Huru ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kuhusu maandamano katika Ukanda wa Gaza wa Palestina, imeitaka Israel kuhakikisha mara moja kuwa kanuni za uwepo wa vikosi vyake vya usalama zinarekebishwa, kwa kulingana na vigezo vya kisheria duniani. Kamisheni hiyo imewasilisha ripoti ya utafiti wake kwa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa baada ya kuchunguza mauaji yote na majeruhi yaliyosababishwa na vikosi hivyo katika eneo la kati ya Israel na Ukanda wa Gaza wakati wa maandamano ya mwaka jana. Ripoti imechunguza kwa makini amri za vikosi vya ulinzi vya Israel kutuma askari na kuchukua hatua zilizosababisha vifo vya waandamanaji wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |