• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuboresha biashara na nchi za nje

    (GMT+08:00) 2019-03-19 18:48:00

    Wizara ya biashara ya China hivi karibuni imefanya mkutano kuhusu uuzaji na uagizaji bidhaa na nchi za nje, na kuzitaka idara mbalimbali za biashara za China kupanua zaidi soko, kuboresha mpangilio katika soko la kimataifa, kuongeza uagizaji bidhaa kutoka nje, na kuboresha mwundo wa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje.

    Waziri wa biashara wa China Bw. Zhong Shan amesema, jambo muhimu katika biashara na nchi za nje ni kudumisha utulivu na kuinua sifa, na kwamba ni lazima kudumisha ukubwa wa maendeleo ya biashara, na kutuliza soko.

    Bw. Zhong Shan amesema, hatua zinazofuata sasa ni kuhimiza uuzaji bidhaa zenye teknolojia ya juu, sifa bora na thamani ya juu, ili kuinua hadhi ya China katika mlolongo wa thamani duniani. Pia China inapaswa kujitahidi kupanua uagizaji bidhaa kutoka nje, kuboresha mwundo wa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje, ili kukidhi zaidi mahitaji ya soko la ndani.

    Ameongeza kuwa, China inaharakisha maandalizi ya maonyesho ya pili ya uagizaji bidhaa kutoka nje, anaamini kuwa maonyesho hayo yatakuwa na fursa nyingi zaidi ya biashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako