• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: TPA yachangia jamii Tanga

    (GMT+08:00) 2019-03-19 20:02:44
    Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), imetenga Sh. milioni 50 kwa Mkoa wa Tanga kuchangia shughuli za kijamii katika miji inayozunguka bandari ikiwa ni mpango wa bajeti ya mwaka 2018/2019.

    Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deodatus Kakoko, alisema fedha hizo ni mpango wa kuchangia kupitia asilimia za mapato yake utakaotolewa katika maeneo muhimu ya kijamii kama elimu na afya.

    Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi mabati 379 ya Shule ya Ufundi ya Tanga alisema pamoja na bati hizo, Mamlaka hiyo itachangia huduma za afya Wilaya ya Pangani.

    Alisema uchangiaji huo ni utekelezaji wa sera ya Bodi ya Mamlaka hiyo na pia jamii inayoishi katika maeneo hususani yaliyozungukwa na Bandari na nchi nzima itanufaika na mpango huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako